Maandalizi ya Kuzaliwa kwa Dayosisi Mpya ya Kahama
- Event
- April 7, 2026
- By —Anglican Tabora
- UTANGULIZI
Kuanzishwa kwa Dayosisi ya Kahama ilijadiliwa na kuamuliwa katika Mkutano wa kumi na mbili (12) wa Sinodi takatifu ya Dayosisi ya Tabora iliyokutana tarehe 16 – 19 Juni, 2024 katika ukumbi wa Canon Nashon Nkugwe – Tabora Manispaa. Ambapo Halmashauri Kuu ya Kanisa Anglikana Tanzania iliyoketi Novemba 2025 Jijini Dodoma iliridhia Kahama kuwa Dayosisi
Pia, tulipewa barua ya idhini ya kuanzisha Dayosisi ya Kahama yenye kumb: KAT/BR/KM/2025/213.
- MIPAKA YA DAYOSISI TARAJIWA YA KAHAMA
Dayosisi tarajiwa ya Kahama itakuwa ndani ya mipaka ya kiserikali ya wilaya tatu zenye ukubwa wa kilometer za mraba 12,506.64. Wilaya hizo ni; Kahama Mkoa wa Shinyanga, Mbogwe na Bukombe – Mkoa wa Geita. Kwa sasa Dayosisi tarajiwa ina mitaa/parishi 18 na wachungaji 20, wainjilisti 38, makanisa 43 na wakristo 6,181.
Dayosisi ya Kahama itaundwa na Dinari za Kahama, Ushirombo na Bukondamoyo.
- SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
- Ununuzi wa nyumba na gari kwa ajlii ya Baba Askofu. Nyumba ipo ndani ya viwanja viwili vilivyounganishwa vilivyopo Lugela Kata ya Nyahanga.
- Tumejenga ofisi za Uaskofu vyumba vitatu katika Kanisa jipya linaloendelea kujengwa.
- Tunaendelea kukusanya fedha na michango mbalimbali kutoka kutoka maparishini na wadau.
- MAMBO YA KUOMBEA
- Kuombea ukamilishwaji wa ujenzi wa ofisi Kuu za Uaskofu
- Ujenzi wa kanisa kuu
- Uchanguzi wa Askofu tarehe 17 Julai, 2026
- Ununuzi wa mavazi ya kiliturujia ya Askofu
Maandalizi ya Kuzaliwa kwa Dayosisi Mpya ya Kahama
Events & News
- Maandalizi ya Kuzaliwa kwa Dayosisi Mpya ya Kahama April 7, 2026
- Confirmation Service at Trinity Church, Parish of Bukondamoyo September 5, 2025
- Help The Anglican Church, Diocese of Tabora Raise Fund for Nyamilangano Parish September 3, 2025
- One House of Our Diocese Was Consumed by Fire and Caused the Whole House to Be Burnt August 22, 2025
- Bishop Dr. Elias Chakupewa, Pastors and Their Spouses During a Retreat in Serengeti National Park August 20, 2025
The Diocese of Tabora was inaugurated on 2nd July 1989. The current Diocesan Bishop is the Rt. Rev. Dr. Elias Chakupewa Mazi who was consecrated and enthroned since 29th May, 2011.



